Kwa ushiriki wa nchi (40): Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zafungua kongamano la kumi na tano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada.

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya Jumanne (3 Shabani 1440h) sawa na (9 April 2019m) ndani ya ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), zimefanya ufunguzi wa kongamano la kumi na tano la Rabiu Shahada, ambalo ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) na nuru za Muhammadiyya katika mwezi huu wa Shabani, chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein –a.s- ni mnara wa umma na suluhisho madhubuti), litakalo fanyika kuanzia mwezi (3 – 7 Shabani).

Hafla ya ufunguzi imepata mahudhurio makubwa ya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya taifa, wakiwemo wawakilishi wa Maraajii Dini na Ataba tukufu pamoja na mazaru takatifu, sambamba na wageni wengi waliokuja kwenye kongamano hili kutoka nchi (40), na waandishi wa habari kutoka vyombo zaidi ya (25), vituo vya luninga, redio, magazeti, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Ataba mbili tukufu.

Halfa ya ufunguzi ilianza kwa kisomo cha Quráni tukufu, iliyo somwa na Sayyid Hussein Halo, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), amesema hua: “Hakika ujumbe wa sasa unatakiwa ujikite katika misingi ya elimu na kujiepusha na maneno ya uchonganishi na ugombanishi, hatumaanishi kutupa misingi ya Dini au madhehebu, kila mtu anahaki ya kukumbatia jambo analo liona ni sahihi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na kuendelea kushirikiana na jamii yake pamoja na taifa lake..”.

Ikafuata kaswida ya mshairi kutoka Misri bwana Ahmadi Bukhiti, halafu ukafuata ujumbe wa wageni ulio wasilishwa kwa niaba yao na Dokta Mustwafa Rashidi Mufti wa Australia na New Zealand na rais wa taasisi ya haki za kibinaadamu chini ya umoja wa mataifa, akasema kua: “Hakika Iraq na raia wake wapenzi, taifa hili lina kila utukufu kwa umma wa kiislamu, huu ndio ukweli wa kihistoria uislamu unatufundisha kumpa kila mtu sifa anayo stahiki..”.

Halafu akazungumza Pr. Krikor Kosach ambaye ni mwandishi na mtafiti wa historia ya miji ya kiarabu na mashariki ya kati, yupo katika kitengo cha Mashariki ya sasa kwenye chuo kikuu cha serikali ya Urusi cha elimu za kibinaadamu, nilipo angalia mazuwaru wa Ataba tukufu za Karbala nimeona nuru katika macho yao isiyo elezeka zaidi ya nuru ya ukarimu wa kibinaadamu..”.

Baada ya hapo mshairi bwana Mahadi Shaakir akasoma shairi lililo shika nafasi ya kwanza katika shindano la mashairi ambalo ni sehemu ya kongamano hili, lililokua likisema: (Shida lakini Hussein).

Ujumbe wa Dokta Ihtisaam Hassan kiongozi wa taasisi ya Mu-ammal katika mji wa Laknau India ukafunga pazia hilo, miongoni mwa aliyosema ni: “Hakika ushindi wa wairaq dhidi ya magaidi wa Daesh uliopatikana kwa utukufu wa fatwa na mwitikio wa wananchi ni fahari kwetu..”.

Hafla ikahitimishwa kwa kaswida na mashairi ya Husseiniyya yaliyo imbwa na Mulla Jaliil Karbalai, tunatarajia jeoni ya leo kutakua na kikao cha kisomo cha Quráni ambacho watashiriki wasomaji wa kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: