Maoni katika picha
Kikao hilifunguliwa na msomaji wa Atabatu Husseiniyya tukufu bwana Osama Karbalai, kisha kikafuata kikosi cha wasomaji wa Qur,ani kutoka Atabatu Husseiniyya tukufu tawi la Ahwaaz, walikua wanaburudisha masikio ya wahudhuriaji baina ya kusoma Qur’ani tukufu na Kaswida, kisha ikaendelea Darul Qur’ani ya Atabatu Husseiniyya tukufu, kupitia mmoja wa wanafunzi wake aitwae Hussein Hajjaar, aliburudisha wahudhuriaji kwa kisomo murua, halafu ukaingia wakati wa Atabatu Radhawiyya tukufu kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran, akasoma Hamiid Shaakir Najaad, na kuhitimisha kwa kisomo cha Mmisri Hamdi Rashidi.
Kuhusu ratiba hii tumeongea na kiongozi wa idara ya habari ya Darul Qur’ani tukufu katika Atabatu Husseiniyya Ustadh Swafaa Silaawi, akasema kua: “Darul Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Husseiniyya inatilia manani kufanya kikao hiki kila mwaka, katika ratiba ya kongamano la Rabiu Shahada, na huwakaribisha wasomaji bora wa kitaifa na kimataifa”.