Hivi ndio masayyid ambao ni watumishi wa Abulfadhil Abbasi walivyo mpongeza Imamu Hussein kwa kuzaliwa ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamezowea kila ifikapo tarehe (4 Shabani), kutoka kwa pamoja wakiwa wamevaa nguo maalumu na kwenda kumpongeza Imamu Hussein (a.s) katika malalo yake takatifu, kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mwaka huu sawa na miaka mingine, baada ya Adhuhuri ya mwezi nne Shabani, ambayo ndio siku alizaliwa mwezi wa familia na mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s), wametoka katika malalo yake tukufu na kuelekea katika malalo ya ndugu yake bwana wa mashahidi wakiwa wamebeba mishumaa na halwa huku wametanguliwa na watu walio beba mauwa, jambo hili ni miongoni mwa turathi za Karbala, wamezowea kufanya hivyo katika matukio ya furaha au matukio muhimu kwao, na miongoni mwa matukio hayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), wamekwenda hadi katika haram ya Imamu Hussein (a.s) na kupokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, ambao huwapokea mauwa na halwa halafu huzigawa kwa mazuwaru waliopo ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s).

Wakati wanatembea walikua wanaimba kaswida na mashairi yanayo onyesha mapenzi na utiifu wao kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), pamoja na kushikamana nao na kufuata mwenendo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: