Katika Atabatu Husseiniyya tukufu na kwa ushiriki wa watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq: Kinafanywa kikao cha uwasilishaji wa mada za kitafiti katika kongamano la Rabiu Shahada.

Maoni katika picha
Watafiti wanaendelea kuwasilisha mada zao katika siku ya pili mfululizo, mara hii kikao kinafanyika ndani ya Atabatu Husseiniyya katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaau (a.s), kikao cha tatu kimefanyika na kuhudhuriwa na watafiti wa ndani na nje ya Iraq.

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati ya maandalizi na kiongozi wa kamati ya majaji iliyo jaji tafiti hizo, Shekh Ammaar Hilali ambae pia ni rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, amesema kuwa kikao hiki ni mwendelezo wa vikao viwili vilivyo fanywa, vyenye mada madhubuti zinazo endana na utukufu wa kongamano hili, kimehudhuriwa na jopo la watafiti pamoja na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai (d.i) na katibu wake mkuu, imewasilishwa mihtasari mitatu ya tafiti kama ifuatavyo:

  • 1- Utafiti wa Sayyid Aqiil Gharwi kutoka India, utafiti wake unasema: (Mimbari Husseiniyya na mambo yasiyo kua na mwisho).
  • 2- Utafiti wa Shekh Ali Jaziri kutoka Saudia, utafiti wake unasema: (Kuangazia kuhusu kumpenda Ali –a.s-).
  • 3- Utafiti wa Shekh Muniir Kadhimi kutoka Iraq, utafiti wake unasema: (Mafunzo ya khutuba za kimalezi katika siku ya Twafu baina ya mtazamo wa kiongozi na tabia za wafuasi).

Kikao kimeshuhudia michango mingi ya maoni kutoka kwa wahudhuriaji, kisha watafiti walio shiriki katika kaikao hiki wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: