Maoni katika picha
Baada ya kusimama watumishi wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) na wageni wa kongamano ikasomwa Quráni tukufu ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, baada ya hapo wakaelekea katika kaburi la bwana wa mashahidi (a.s) kufanya ziara na kutoa miito ya Imani iliyo kua ikisema:
Wito wa Aqida kwa walio changanikiwa ….. Hussein Hussein Hussein Hussein
Mbainishaji wa ujumbe wa Mitume na Manabii …… katunzwa na watawala wa Karbala
Zikafuatia kaswida za kidini.
Tukio hili la kiibada limepongezwa na kusifiwa na wageni wa kongamano, nalo hufanywa kila siku katika muda wa kazi baina ya zamu mbili ya asubuhi na jioni, kwa ajili ya kuhuisha utiifu kwa Imamu Hussein (a.s) pamoja na kujikumbusha malengo makuu yaliyo sababisha ajitolee damu na roho yake, ambayo ni uislamu na kufatwa sharia zake tukufu pamoja na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).