Maoni katika picha
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Jafari Mussawiy (d.t) pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya, kilifunguliwa kwa Quráni tukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ikaanza kuwasilishwa mihtasari ya mada za kitafiti kama ifuatavyo:
Utafiti wa kwanza ulikua wa Shekh Iswamul Hamdi/ kutoka Yemen, utafiti wake unasema: (Riwaya za utukufu wa Imamu Hussein –a.s- kutoka kwa Maimamu watakasifu).
Utafiti wa pili ulikua wa Shekh Muslim Radhwai/ kutoka Afghanistani, utafiti wake unasema: (Utafiti wa kifiqhi katika vitabu vya Maqtal Husseini.. kitabu cha Iksiri Ibadaat cha Darbandi kama mfano).
Utafiti wa tatu ulikua wa Dokta Haidari Masjidi/ kutoka Iran, utafiti wake unasema: (Utafiti mpya katika riwaya za tahriif).
Wahudhuriaji walitoa maoni na michango mbalimbali, baada ya hapo watafiti walio shiriki katika kikao hiki wakapewa zawadi.