Kwa mara ya kwanza katika sekta ya maonyesho nchini Iraq: Maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala yanatoa huduma ya (Uliza kitabu chako).

Maoni katika picha
Jambo jipya ambalo linafanywa kwa mara ya kwanza katika sekta ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Iraq, kutokana na juhudi za wasimamizi wa maonyesho haya, wameanzisha huduma ya (Uliza kitabu chako) ambayo inamrahisishia mtu anayetaka kutafuta kitabu maalumu kilichopo katika taasisi au kituo kinacho shiriki kwenye maonyesho haya.

Yamekusanywa majina ya vitabu vyote vinavyo shiriki katika maonyesho haya na kuandikwa sehemu moja, nayo ni zaidi ya elfu thelathini na tano (35,000) katika taasisi na vitu vya usambazaji (140) vinavyo shiriki, pia huduma hii inamuelekeza mtu sehemu kilipo kitabu husika kwa ajili ya kumuondolea usumbufu wa kukitafuta.

Utanufaika vipi na huduma hii?

Namna ya kunufaika na huduma hii, mfuate mhudumu anayefanya kazi katika sekta hiyo, inayo itwa (Muyassir), kisha mpe jina la kitabu au muandishi wa kitabu unacho hitaji, mtumishi hiyo ataliingiza katika ukurasa wa maina kisha atakupa karatasi inayo kuelekeza jina kamili la kitabu na muandishi wake na jina la taasisi au kituo kilipo kitabu hicho.

Watumishi wa huduma hii wanatoa maelekezo kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyo elekeza vituo vinavyo shiriki katika maonyesho, sambamba na uwepo wa mabango yanayo onyesha ramani ya sehemu ilipo huduma ya (uliza kitabu chako), mabango hayo yamewekwa sehemu mbalimbali katika uwanja wa katikati ya haram mbili yanapo fanyika maonyesho ya vitabu ya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: