Maoni katika picha
Hafla hiyo ilihudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Jafari Mussawi (d.t) na jopo la wajumbe wa kamati ya viongozi wa Ataba mbili tukufu, pamoja na wageni wa kongamano la Rabiu Shahada na washindi wa shindano hilo, baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ulifuata ujumbe wa kamati iliyo simamia shindano hilo, ulio wasilishwa na Dokta Twalali Kamali, akabainisha malengo ya shindano hilo na vigezo walivyo tumia katika kushindanisha vitabu hivyo, halafu yakatangazwa majina ya washindi watatu wa mwanzo na wakapewa zawadi pamoja na washindi wengine saba wanao wafuatia, nao walikua kama ifuatavyo:
Washindi watatu wa mwanzo:
- 1- Dkt: Muhammad Idani Al-Abadi / kulinda historia ya Ashura, kujibu shubha za ibun Taimiyya kuhusu mambo yaliyo tokea Twafu.
- 2- Nuru Mahadi Kaadhim Saaidiy/ alama za maadhimisho ya Husseiniyya – uchunguzi katika turathi za kidini na kijamii.
- 3- Alaa Jabri Muhammad Musawiy/ upekee wa hadhi ya Imamu Hussein (a.s) – misingi – vigezo – uwezo.
Washindi waba waliofuatia ni:
- 4- Muhsin Wahibu Abdunaswiri Sa’dawi/ Imamu Hussein (a.s) ni mrithi wa Manabii.
- 5- Yusufu Mudanin/ fikra za kibinaadamu na athari za kimalezi kwa Imamu Hussein (a.s).
- 6- Ahmadi Alayuwi/ sifa za uongozi katika harakati ya Imamu Hussein (a.s).
- 7- Haadi Abdunabi Tamimi/ uhai wa Imamu Hussein na harakati yake tukufu.
- 8- Abbasi Ismaili/ Imamu Hussein katika hatua ya utoto.
- 9- Swalehe Twaaiy/ Hussein ni hakimu.
- 10- Aalaau Swafi Khadhwiri/ Imamu Hussein katika fikra za Abbasi Al-Aqaad.