Kongamano la kitamaduni Rabiu Shahada linaangalia fikra kutoka zaidi ya nchi nane za kiarabu katika mkutano wa wanawake.

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada linalo endelea sasa hivi, kama ilivyo toa nafasi kwa watafiti wa kiume, pia haikuwasahau watafiti wa kike, (iliandaa mkutano wa kuwasilisha mada za kitafiti kwa wanawake ulio fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: Mwanamke baada ya Ashura.. kuangalia changamoto za sasa), washiriki wa program hii walikua (37) kutoka nje ya Iraq na watafiti (44) kutoka ndani ya Iraq.

Kikao cha kuwasilisha mada za kitafiti kimefanyika ndani ya ukumbi wa Sayyid Auswiyaa (a.s) katika Atabatu Husseiniyya, kilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha ikawasilishwa mihtasari ya mada za kitafiti, kama ifuatavyo:

Mada ya kwanza: Dokta Raghida Misriy kutoka Lebanon, mada isemayo: (Familia na mwanamke wa kiislamu.. uhalisia na changamoto).

Mada ya pili: Bibi Zakia Sayyid Ali Sharafu kutoka Baharain, mada isemayo: (Nafasi ya mwanamke katika kuleta mabadiliko na islahi).

Mada ya tatu: Dokta Hanaa Sudani kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran, mada isemayo: (Nafasi ya mwanamke kisiasa… vita ya Twafu kama mfano).

Kikao kilipambwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, watoa mada walijibu maswali na kutoa ufafanuzi pale ulipo hitajika, kikao kikafungwa kwa kutoa zawadi kwa wale walio shiriki kuwasilisha mada.

Kumbuka kua miongoni mwa malengo makubwa ya mkutano huu ni:

  • 1- Kuangalia mwenendo wa Maimamu (a.s) namna walivyo shirikiana na mwanamke katika vita ya Twafu na baada ya vita.
  • 2- Kuonyesha nafasi ya mwanamke katika uislamu.
  • 3- Kuangalia changamoto za sasa alizo nazo mwanamke.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: