Nukta muhimu alizo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) tarehe (6 Shabani 1440h) sawa na (12 April 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai (d.i), ameongelea nukta nyingi za kimaadili na kimalezi zinazo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa nukta hizo ni:

 • - Kuna mambo yanatishia mmomonyoko wa maadili katika jamii na mshikamano.
 • - Kuna misingi ya kimaadili na kidini inayo toa mwongozo wa kusambaza vitu katika mitandao ya kijamii.
 • - Misingi hiyo ikifatwa mitandao ya mawasiliano ya kijamii itakua na manufaa na isipo fatwa itakua na madhara kitamaduni, kimaadili na kijamii.
 • - Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwetu katika zama hizi ni kuturahisishia nyenzo za mawasiliano ya aina mbalimbali baina yetu.
 • - Neema hii inaweza kubadilika kawa balaa tusipo ongozwa na misingi ya kidini na kimaadili itakayo tufanya tuitumie vizuri na kupata manufaa makubwa.
 • - Fikiri na tafakari hatima ya unachotaka kuweka kwenye mitandao ambacho kinaweza kifikia mamilioni ya watu.
 • - Lazima kila mtu mwenye akili na mshika Dini afikiri kwa kina na kuuliza nafsi yake kuhusu kitu anacho taka kuweka kwenye mtandao.
 • - Kila unacho taka kuweka kwenye mtandao kipime katika akili na sheria pamoja na maadili ya kibinaadamu, kikiwa kina manufaa kiweke na kama hakina kiache.
 • - Tusifanye haraka kusambaza mambo kwenye mitandao.
 • - Mitandao ya mawasiliano ya kijamii imejaa imejaa mambo na habari zisizokua na vyanzo vya kueleweka na nyingi hazina nia nzuri na zinashambulia au zinadhuru watu wengine.
 • - Miongoni mwa mambo yasiyo faa kabisa ni kutafuta kasoro za watu na kuzirusha kwenye mitandao.
 • - Kuna baadhi ya watu huficha makosa yao kwa kuwashambulia wale wanaotofautiana nao kifikra, kiimani au kidini.
 • - Uzushi na matusi haviruhusiwi kisheria katika mjadala wa kielimu na kiimani, unatakiwa kutumia hoja na dalili.
 • - Hakika kalamu na maandishi ni ulimi wa pili.
 • - Tunaulimi huu tunaotumia kuongea na ulimi wa pili ni kalamu na maandishi, mwislamu wa kweli ni yule ambaye waislamu watasalimika kutokana na ulimi wake, kalamu na maandishi yake.
 • - Jitahidi uwe mtu mwenye manufaa katika ulimwengu wa mitandao ya mawasiliano ya kijamii na wala usiwe mtu mwenye madhara kwa wengine unaye sambaza uovu.
 • - Usitumie mitandao ya mawasiliano ya kijamii kutukana na kushamgulia watu pamoja na kusambaza mambo machafu.
 • - Jihadhari na matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii, na uchukue tahadhari ya wavamizi wa mitandaoni.
 • - Chini ya mwanvuli wa uhuru na haki ya kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii kuna watu wanafanya mambo ya kishetani na ya haram.
 • - Msiwape nafasi ya kutumia taarifa zenu watu wanao fanya mambo ya kishetani na ya haram.
 • - Ni jukumu la kila mtu anaye jitambua na familia kua na tahadhari kubwa na kuhakikisha hawawapi nafasi watu waovu ya kutumia taarifa zao, jambo ambalo litawanyima amani ya nafsi na utulivu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: