Mchana wa siku ya Ijumaa, msafara wa shehena zaidi ya (200) ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia walia athirika na mafuriko uliwasili kwenye mji wa Misaan, kupitia idara ya ustawi wa jamii, (Chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito ulio tolewa na kiongozi mkuu wa kisheria mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi).
Shekh Abbasi Akaashi mkuu wa idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Msafara huu ni sehemu ya kuitikia maombi ya wananchi na kutekeleza matakwa ya Marjaa Dini mkuu na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kutoa msaada wa haraka kwa walio athirika na mafuriko”.
Sayyid Hassan Saáduni kiongozi anaye wakilisha kikosi cha Abbasi cha wapiganaji katika mji wa Misaan amesema kua: “Msafara wa shehena ya misaada ya Atabatu Abbasiyya imetoka katika mikoa kumi na moja, chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi, msafara huo una bidhaa mbalimbali za kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika mkoa wa Misaan”.
Akasema kua: Atabatu Abbasiyya tukufu na idara zake za ustawi wa jamii imeitikia wito kwa haraka wa kwenda kusaidia waathirika wa mafuriko.
Pia wahandisi wake wanafanya kazi ya kuondoa maji ya mafuriko katika makazi ya watu usiku na mchana kwa ajili ya kuwalinda na mlipuko wa magonjwa, mkuu wa madaktari wa dharura katika mji wa Misaan Dokta Ghazwaan Maidi Kaadhim ameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa misaada ya kibinaadamu inayo toa katika mkoa wa Misaan, akasema kua: “Hakika tumepewa msaada mkubwa sana na utasaidia kupambana na changamoto za mafuriko”.
Akasema kua, karibu familia 2000 zimeathirika na mafuriko haya, ambayo yameingia katika eneo kubwa la makazi ya watu katika mkoa huu, akasema kua vyombo vya kutoa huduma kwa raia vimedhibiti hali kwa kiasi kikubwa.