Atabatu Abbasiyya tukufu yaeleza juhudi inazofanya katika mkoa wa Waasit na Misaan.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeitikia kwa haraka wito wa kuomba msaada uliotolewa na wakazi walio athirika na mafuriko katika mkoa wa Waasit ba Misaan, kupitia vitengo vyake na idara ya ustawi wa jamii pamoja na mawakibu za kutoa huduma zilizo chini yake, imetuma misaada ya kibinaadamu katika mikoa tuliyo taja, bado kuna juhudi kubwa zinazo endelea hivi sasa za kutuma misaada zaidi kwa waathirika wa mafuriko katika mikoa hiyo, kwa kushirikiana na idara za ustawi wa jamii za mikoa mbalimbali.

Sambamba na misaada hiyo jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wapo huko kusaidia uokozi wa watu walio zungukwa na maji, kufuatia agizo la ghafla lililo tolewa na viongozi wa kikosi cha Abbasi, pia kimetumwa kikosi maalumu cha kupambana na nguvu za maji (mito), na imewataka wapiganaji wa hakiba waliopo katika mikoa hiyo washirikiane na serikali za maeneo hayo katika kupambana na tatizo hilo.

Hali kadhalika taasisi ya Nurul Hidaya ambayo ipo chini ya idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa vikapu (120) vya misaada pamoja na matandiko, nguo na vifaa vya majumbani kwa waathirika wa mafuriko.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: