Mubaligh Omari Jarati: Hakika tuliyo sikia kuhusu Iraq yanatofautiana kabisa na tunayo yaona hivi sasa.

Maoni katika picha
Mubaligh Omari Jarati ambaye ni muasisi wa madrasat Irshadi katika Jamhuri ya Averekosti amesema kua: “Hakika tuliyo sikia kuhusu Iraq yanatofautiana kabisa na tunayo yaona hivi sasa”.

Ameyasema hayo alipo wasili katika mji wa Karbala kuitikia mwaliko aliopewa na Ataba mbili tukufu wa kuja kushiriki katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shaha ya kumi na tano.

Akabainisha kua: “Katika mji wa Karbala tumekuta ushirikiano na maelewano wala hakuna ubaguzi, na hiyo ndio misingi ya maisha ya hapa, kama kungekua na ardhi nyingine duniani ambayo ni tukufu zaidi ya Karbala bado ingeendelea kua Karbala ndio kilele cha utukufu, kwa sababu ni ardhi iliyo muhifadhi Mjukuu wa Mtume (a.s) na wafuasi wake”.

Akaongeza kusema kua: “Kupitia kongamano hili nimeona Karbala ni mji wenye watu wenye fikra tofauti na Dini tofauti wanao ishi kwa pamoja bila ubaguzi wala mifarakano”. Akasema kua atakwenda kusimulia aliyo yaona katika nchi yake: “Niyiyo yaona nitakwenda kusimulia kwa waislamu wote wa Averekosti na sehemu zote nilizo tembelea, nitakwenda kusema uhalisia wa waislamu wa Iraq na kuondoa picha mbaya wanayo pewa na vyombo vya habari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: