Uongozi mkuu wa mazaru za kishia umeshiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya kumi na tano yanayo fanyika Karbala sambamba na Ataba zingine pamoja na vituo vya usambazaji vya ndani na nje ya Iraq, ulikua na nafasi kubwa katika maonyesho haya, na walipewa nafasi maalumu.
Kitengo cha uhusiano kimeshiriki pamoja na mazaru kadhaa kutoka mikoa tofauti, miongoni mwa mazaru hizo ni: mazaru ya Alawiyya Sharifa bint Imamu Hassan Almujtaba (a.s), mazaru ya Swahaba Maitham Tammaar, mazaru ya Zaidu Shahid, mazaru ya Sayyid Ibrahim Ghamru, mazaru ya Rashidi Hajriy na mazaru ya Nabii Dhulkifli (r.a), wakiwa na vitabu mbalimbali, vya dini, utamadu, aqida, jamii pamoja na vipeperushi vinavyo elezea mazaru tukufu, katika maonyesho haya zimeshiriki zaidi ya taasisi (150) za usambazaji wa vitabu kutoka (Iraq na katika nchi za kiarabu na kiajemi), pia maonyesho haya yameshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru waliokuja kuyatembelea na wakaonyesha kuridhika na vitabu vilivyo kuwepo.
Kwa mujibu wa matawi yaliyo shiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala yanatoa fursa ya kuwasiliana kwa wataalamu wa fani mbalimbali, pamoja na kuimarisha uhusiano wa taasisi za kielimu, kijamii na kimalezi.