Shekh Maliki Muqadam kutoka Ufaransa ameonyesha kufurahishwa na kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano, akasema kongamano hili ni muhimu duniani na kuna haja kubwa ya kufanywa kongamano la aina hii kutokana na mazingira tunayoishi katika ulimwengu wa sasa.
Ameyasema hayo baada ya kuwasiri katika mji wa Karbala kuitikia mwaliko wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wa kuja kushiriki katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na tano.
Akaongeza kua: “Kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na tano ni mfano mwema ya kuishi pamoja kwa Amani watu wa dini tofauti, linaonyesha utamaduni wa kuvumiliana baina ya watu, leo duniani tunahaja kubwa sana ya kufanywa makongamano kama haya, kwa sababu tunaishi katika zama zenye watu waliojaa chuki za kidini, jambo linalo pelekea kujiuliza maswali mengi na kutafakari njia sahihi ya kuondoa tatizo hilo na kuwafanya watu waishi kwa amani na usalama pamoja na kutofautiana tamaduni na dini zao”.
Akamaliza kwa kusema: “Hakika kongamano la Rabiu Shahada ni muhimu sana katika zama hizi, lipepokea wageni kutoka nchi (40), zimeshiriki Dini tofauti pamoja na taasisi za haki za binaadamu pamoja na wasomi na watafiti wa kimataifa”.
Akasema: “Kongamano hili limeonyesha wazi umuhimu wa kufuata misingi ya uadilifu na usawa katika Dini ya kiislamu, binaadamu wote tuko sawa mbele ya haki na wajibu”.