Katika mkakati wake wa kusaidia, jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wameweza kuzuwia maji yasiingie katika makazi zaidi ya watu kwenye mkoa wa Misaan na Waasit iliyokubwa na mafuriko kwa siku kadhaa sasa.
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi amesema kua: “Jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi limefanikiwa kuzuwia maji yasiingie katika makazi zaidi ya watu na mashamba kwa kiasi kikubwa, kwenye maeneo ambayo yalikua yanahatari ya kuzama kwa mafuriko”.
Jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi lilikwenda katika mkoa wa Misaan na Waasit tangu siku mbili zilizo pita, na wakaanza kazi kwa kushirikiana na vikosi vilivyopo katika mikoa hiyo, wamefanya kazi usiku na mchana bila kupumzika.
Fahamu kua mawakibu za kutoa huduma zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu zimepeleka shehena (200) ya misaada ya kibinaadamu katika mkoa wa Misaan siku ya Ijumaa.