Wasomaji wa Qur’ani wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata nafasi za juu katika mashindano ya Qur’ani ya kimataifa awamu ya 36.

Maoni katika picha
Wasomaji wa Qur’ani wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka katika Maahadi ya Qur’ani, wamepata nafasi za juu katika mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani tukufu awamu ya (36), yaliyo malizika hivi karibuni katika jamhuri ya kiislamu ya Iran mjini Teheran na kushiriki nchi (82) za kiarabu na kiajemi.

Matokeo ya mashindano baada ya kushinda hatua za awali (makundi), msomaji bwana Muhammad Ridhwa Salmaan amepata nafasi ya tatu katika usomaji wa tahqiqi, huku msomaji Muslim Aqiil akipata nafasi ya nne katika usomaji wa Tartiil wa kikundi cha wanafunzi wa masomo ya Dini, na Shekh Muhammad Ambaari akapata nafasi ya tatu katika mashindano ya wanafunzi wa Dini kwenye sekta ya khutuba za Qur’ani.

Kumbuka kua mashindano haya yalikua na washiriki (620) kutoka nchi (82) ni moja ya mashindano ya Qur’ani makubwa duniani, maandalizi ya mashindano haya yalianza muda mrefu, yamefanyika mashindano mengi ya Qur’ani ambayo Atabatu Abbasiyya ilikua inashinda na ndio maana ikapata nafasi ya kuiwakilisha Iraq katika mashindano haya matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: