Atabatu Abbasiyya tukufu na mkoa wa Muthanna wanafanya makubaliano ya kufanya miradi ya kutoa huduma katika mkoa huo.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu na serikali ya mkoa wa Muthanna wanafanya makubaliano kuhusu utekelezaji wa miradi ya kutoa huduma, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ilinzi na Amani katika mkoa huo.

Yamefanyika hayo katika ziara iliyo fanywa na mkuu wa mkoa Ustadh Ahmadi Manfi Jawaad ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika ziara yangu ni sehemu ya makubaliano ya mwisho na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilicho tembelea mkoa wetu katika mradi wao wa Alwafaa lisamaawah”.

Akabainisha kua: “Walikutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) wakajadili kuhusu Muthanna, na namna ya kuweka miradi ya kiuchumi na kusaidia mkoa huo kwa kushirikiana na serikali ya mkoa”.

Akabanisha kua: “Katika majadiliano hayo Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alishauri kuchimbwa handaki lenye urenfu wa (km 320) katika mkoa wa Muthanna”, akaonyesha umuhimu wa kutumia vizuri jangwa la samaawah katika kuimarisha ulinzi na usalama, ukizingatia kua jambo hilo linakubaliwa na serikali ya mkoa, pamoja na kujenga barabara ya (Yaa Hussein) kwa kushirikiana baina ya Ataba tukufu na mkoa wa Muthanna. Akasema kua ziara hii ni mwanzo mpya wa mkoa wa Muthanna.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Muthanna bwana Sami Sauud amesema kua: “Hakika kuja kwake Karbala kwa ajili ya kuongea mubashara (moja kwa moja) na mkuu wa kikosi cha Abbasi Shekh Maitham Zaidi kuna faida nyingi”.

Kumbuka kua makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya ulinzi na utowaji wa huduma kati ya mkoa wa Muthanna na kikosi cha Abbasi yapo katika hatua za mwisho, yalianza kufanyika tangu viongozi wa kikosi cha Abbasi walipo tembelea mkoa wa Muthanna kwenye mradi wa Alwafaa lisamaawah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: