Maoni katika picha
Kama kawaida katika siku za ziaya hufunguliwa madirisha ya nje kwa ajili ya kugawia chakula, kutokana na ongezeko kubwa la watu amboa hujaa kwa ajili ya kupata chakula cha baraka itokayo kwa mnyweshaji wenye kiu Karbala, pia chakula hutolewa mchana baada ya Dhuhuraini, muda huo idadi kubwa ya mazuwaru huhitaji chakula, chakula hutolewa kutokana na wingi wa mazuwaru.
Fahamu kua mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hutoa chakula kila siku kwa mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya, na katika siku za ziara maalum hufungua madirisha ya nje kwa ajili ya kugawa chakula kwa mazuwaru wengi zaidi na kuwafanya wapate baraka za chakula cha mwenye malalo hii takatifu.