Kiongozi wa jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Muhammad Karim amesema kua: “Jopo la wahandisi wa kikosi cha Abbasi bado linaendelea kufanya kazi mbalimbali katika mkoa wa Misaan, kwa ajili ya kuzuwia maji yasifike katika nyumba za watu na kuzuwia mafuriko”.
Akasema kua: “Kazi inaendelea vizuri, mkuu wa mkoa wa Misaan ameombwa kuongea na wananchi wake na kuwaambia kuwa mafuriko yamedhibitiwa hakuna hatari ya mafuriko tena”.
Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kilituma wahandisi wake katika mkoa wa Misaan kwenda kusaidia utatuzi wa mafuriko, na kikatuma idara za ustawi wa Jamii pamoja na vitengo vya watoa huduma kwenda kutoa misaada mbalimbali ya kibinaadamu kwa waathirika wa mafuriko hayo.