Kwa mara ya kwanza Mashariki ya kati: Uzinduzi wa mtambo wa kutibu kwa kutumia mionzi kwenye hospitali ya rufaa Alkafeel.

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya imetangaza uzinduzi wa mtambo wa kutibu kwa kutumia mionzi, chini ya usimamizi wa Dokta Adnani Zaidi bingwa wa maswala ya mionzi kwa kushirikiana na madaktari wengine walio bobea katika sekta hiyo.

Magonjwa yanayo tibiwa na mtambo huo ni:

  • 1- Uvimbe mbaya, miongoni mwake ni: (umimbe wa ini, bandama, figo, na sehemu zingine ndani ya mwili na aina hii huweza kusambaa katika mwili).
  • 2- Uvimbe mzuri, miongoni mwake ni: (uvimbe unao onekana kwa nje, uzuri wake ni kwamba hausambai sehemu nyingine ya mwili na hutibiwa kwa kutumia kuondoa sehemu yenye tatizo -qastwara-).
  • 3- Matibabu ya kuondoa sehemu yenye tatizo (qastwara): hutumika kwa kutibu maradhi mbalimbali, kama vile:



Kuondoa sehemu zenye tatizo kabla ya kufanya upasuaji mkubwa, kama vile uvimbe wa kwenye ubongo na kwenye figo.



Kuondoa uvimbe wa kwenye njia ya uzazi.



Kuondoa uvimbe kwenye mishipa ya damu inaweza kua kwenye ubongo au sehemu nyingine ya mwili.



Kuondoa uvimbe wa miguuni.



Kuondoa uvimbe kwenye ubongo.



Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa mbili jioni (07730622230 / 07602329999 / 07602344444), Tunawatakia afya njema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: