Miongoni mwa vikao vyake vya kimalezi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, idara ya tabligh chini ya kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya darasa mjadala kwa wanafunzi wa kitivo cha utawala na uchumi wa chuo kikuu cha Karbala, kilichokua na anuani isemayo: (Uzuri wa tabia njema).
Kikao hicho kiliongozwa na Shekh Saadi Marzuuk kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya ukumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi, mada iliyo zungumzwa ni umuhimu wa tabia njema katika maisha ya mwanaadamu hasa kwa waislamu, kwani Mtume na Maimamu watakasifu (a.s) wamesisitiza sana swala la tabia njema, na kufafanua kwa kina uzuri wa tabia njema, hakika uzuri wa mtu ni tabia zake mbele ya watu na namna anavyo ishi nao, uzuri wa mtu haupimwi kwa mavazi na umbo peke yake, bali huzingatiwa tabia yake mbele ya watu.
Washiriki walipewa nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu mada iliyo tolewa, na mtoa mada akajibu na kufafanua zaidi, pia wanafunzi waliulizwa maswali na wale walio jibu vizuri wakapewa zawadi.
Wanafunzi wa kitivo cha utawala na uchumi wameishukuru idara ya tabligh kwa kufanya kikao hiki, wakasema kua wamepata faida kubwa, pia ni nafasi nzuri ya kutoa ukumbusho kwa vijana na wanafunzi wa chuo kuhusu umuhimu wa tabia njema katika maisha ya shule na kazi, wakasema kua jambo hili sio geni kufanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani imekua mstari wa mbele katika kuwajenga wanafunzi kielimu na kimaadili.