Wakeni wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada wanatembelea Ataba tukufu za Iraq.

Maoni katika picha
Wageni wa kongamano la Rabiu Shahada ya kumi na tano lililo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Imamu Hussein –a.s- ni mnara wa umma na suluhisho madhubuti), wanatembelea Ataba tukufu za Iraq, ambazo ni Atabatu Alawiyya, Atabatu Askariyya na Atabatu Kadhimiyya tukufu pamoja na malalo ya Sayyid Muhammad (a.s) katika mji wa Dujail.

Ziara hizo zipo ndani ya ratiba waliyo andaliwa wageni wa kongamano la Rabiu Shahada lililo isha siku ya Jumamosi ya mwezi (7 Shabani 1440h) sawa na (13 April 2019m) baada ya kufanyika kwa siku tano zilizo jaa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatembeza katika miradi ya Ataba mbili tukufu, wageni hao wamefurahishwa sana na huduma mbalimbali zinazo tolewa na Ataba, kwani Ataba zimekua kiini cha mambo ya dini, elimu na utamaduni.

Wameshukuru sana kupata nafasi ya kushiriki katika ziara ya kutembelea Ataba tukufu za Iraq, wakasema hi ni heshima kubwa waliyopewa kabla ya kumaliza safari yao hapa Iraq, pamoja na kufahamu maendelea yaliyopo katika Ataba tukufu ambazo zimekua vinara katika mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: