Mwezi kumi na moja Shabani alizaliwa mtu anayefanana zaidi na Mtume (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi kumi na moja Shabani ulizaliwa mwezi miongoni mwa miezi ya Alawiyya Ali Akbaru (a.s), alikua mtu mtukufu sana katika uislamu, nyota yake iliangaza katika anga ya Twafu na jangwa la Karbala akipambana kwa ajili ya uislamu na misingi ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Jina lake kamili ni: Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s). jina lake la kuniya anaitwa: Abulhassan. Mama yake anaitwa: Laila binti Abu Urwah bun Masoud Athaqafiy.

Alizaliwa katika nyumba ya imani na uchamungu.. anaheshima kubwa kwa Ahlulbait (a.s), jambo hilo linaonekana wazi katika siku ya Ashura alipo toka kwenda kupigana baada ya kuomba ruhusa kwa Imamu Hussein (a.s), Imamu alimwangalia halafu akatokwa na machozi akainua mikono yake na akasema: (Ewe Mola shuhudia watu hawa wanapigana na kijana anayefanana zaidi na Mtume (s.a.w.w) kimaumbile, tabia na kuongea, tulikua tunapo mkumbuka Mtume tunamwangalia yeye, ewe Mola wazuilie baraka za ardhi na uwafarakishe na kuwachana chana, uwafanye wawe makundi makundi, wala usiwaridhie milele, hakika walitwita kutunusuru kisha wametugeuka na kutuua), huo ndio utukufu wa Ali Akbaru (a.s) kwa baba yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Katika ziara tukufu Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Kwa baba yangu wewe na mama, uliye jinjwa na kuuwawa bila kosa, namlilia Allah ewe kiongozi wangu Ali Akbaru katika sehemu hii na heshima kubwa uliyo nayo).

Miongoni mwa sifa zake (a.s) alikua mzuri wa sura, anafanana zaidi na Mtume Muhammad (s.a.w.w), umbo, tabia na kuongea. Na alirithi ushujaa kutoka kwa babu yake kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), alikua na kila aina ya sifa nzuri kama wazazi wake watakasifu wanaojulikana kwa zuhudi, ibada, ukarimu, kuwapa chakula masikini na kukirimu wageni.

Kaburi lake tukufu lipo upande wa miguu ya Imamu Hussein (a.s), imesunuwa kusimama upande wa miguu wakati wa kusoma ziara, na kumzuru Ali bun Hussein utasoma ziara hii: ((Amani iwe juu yako ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Nabii wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yako ewe mtoto wa kiongozi wa waumini, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Hussein Shahiid, amani iwe juu yako ewe madhulum na mtoto wa madhlum, Mwenyezi Mungu awalaali walio kuuwa, na awalaani waliokudhulumu, na awalaani watakao sikia (uliyo fanyiwa) na wakaridhia)).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: