Maahadi ya Qur’ani tukufu inatoa wito kwa taasisi zote za Qur’ani zije kushiriki katika mashindano ya Qur’ani ya vikundi awamu ya tano.

Maoni katika picha: miongoni mwa picha za mashinda
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya, imetoa wito kwa taasisi zote za Qur’ani za hapa Iraq zinazo penda kushiriki katika mashindano ya Qur’ani ya vikundi ya awamu ya tano, yatakayo anza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Idara imesema kua uandikishaji utafanywa katika ofisi za Maahadi ya Qur’ani ndani ya Atabatu Abbasiyya, au katika matawi yake ya (Bagdad, Najafu, Baabil na wilaya ya Hindiyya), au katika linki na vikundi vya Qur’ani katika mikoa mingine, tambua kua mashindano yataanza mwezi (28) Shabani hadi mwezi (14) Ramadhani.

Kila mkoa unahaki ya kuteua vikundi viwili pamoja na rais wa ugeni wao kutoka nje ya washiriki, pia sio vibaya kuchagua kikundi cha tatu kwa tahadhari, kila kikundi kiwe na: (msomaji, aliye hifadhi juzuu kumi za mwanzo, mtu anayefahamu tafsiri –itatumika tafsiri Amthal- juzuu mbili la 22 na 23).

Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo: 07729728488 – 07800119249.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: