Makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu Allawiyya na Abbasiyya wanajadili njia za kuongeza ushirikiano.

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) ametembelea malalo ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), baada ya kufanya ziara na kuomba dua alikwenda katika chumba cha wageni ndani ya Atabatu Alawiyya tukufu, akapokewa na katibu mkuu wa Ataba hiyo Mhandisi Yusufu Shekh Radhi.

Wakazungumza na kujadiliana mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na njia za kuongeza ushirikiano baina ya Ataba mbili tukufu, kwa lengo la kuboresha huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika mji wa Najafu na Karbala tukufu.

Mwisho wa ziara hiyo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu aliagwa kwa furaha kama alivyo pokelewa, na wakaomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kumtumikia kiongozi wa waumini (a.s) kwa kuwawezesha kufanya kazi yao ya kuwahudumia mazuwaru wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: