Kituo cha utamaduni wa familia kinaandaa mashindano ya visa vifupi na kimetoa wito wa kushiriki katika mashindano hayo.

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanyika kwa shindano la (mradi wa hayaatu), shindano maalum kwa wasichana peke yake, wenye umri kati ya miaka (15-30).

Na kimetangaza masharti ya shindano, ambayo ni:

  • - Maudhui ya kisa itokane na maudhui zifuatazo: (familia – mtoto – kisa cha mafanikio ya mwanamke – maendeleo ya kielimu – kujiendeleza – maisha ya ndoa).
  • - Tarehe ya mwisho ya kupokea visha vitakavyo shiriki ni (21 Mei 2019m).
  • - Matokeo yatatangazwa tarehe (10 Juni 2019m) katika hafla maalum itakayo fanywa na kituo.
  • - Zimeandaliwa zawadi za washindi watatu wa mwanzo, mshindi wa kwanza atapewa dinari (300,000) laki tatu za kiiraq, mshindi wa pili dinari (200,000) laki mbili za kiiraq na mshindi wa tatu dinari (150,000) za kiiraq.
  • - Visa vyote vitumwe katika vyuo vikuu na kwenye shule za sekondari au katika baruapepe ifuatayo (thaqafaasria@gmail.com).

Kwa maelezo Zaidi wasiliana nasi kwa simu ifuatayo: 07828884555 (Whatsapp – telegram – viber). Fahamu kua mashindano haya ni kwa wanawake tu.

Kumbuka kua kitengo cha utamaduni wa familia ni moja ya vituo vinavyo fundisha maadili ya familia, ofisi zake zipo katika mkoa mtukufu wa Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) katika jengo la kituo cha Swidiqah mtakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: