Mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji amewasili katika mkoa wa Misaan kuangalia kazi za wahandisi ambao wapo huko kwa siku kadhaa wakipambana na mafuriko, amepokelewa na mkuu wa mkoa Ustadh Ali Dawwai na kuangalia hali ilivyo katika utowaji wa misaada ya kibinaadamu.
Msemaji wa kikosi amesema kua Zaidi amefika hadi sehemu yanakopita maji ya mafuriko kwenye mashamba ya upande wa mashariki ya mji wa Karidi, mkuu wa mkoa amekishukuru sana kikosi cha Abbasi kwa kazi kubwa waliyo fanya ya kuzuwia maji yasienee kuingia katika makazi ya watu.
Zaidi akasema kua kikosi hicho kimekuja kutokana na amri ya Marjaa Dini mkuu pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na kuja kuangalia na kutoa misaada inayo hitajika sambamba na kuleta jopo la wahandisi kuja kuokoa miji hii.
Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilituma jopo la wahandisi katika mkoa wa Misaan, pia kiliwataka askari wake wa hakiba waliopo katika mkoa huo kuwasaidia wananchi, idara za ustawi wa jamii zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu zilituma msafara wa kutoa misaada ya kibinaadamu katika mkoa kipenzi wa Misaan.