Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (13 Shabani 1440h) sawa na (19 April 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), ameongea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa aliyozungumza ni:

 • - Misingi ya malezi haihusu kundi fulani pekeyake, ndio.. inawezekana baadhi ya makundi yakawa ni makamilishaji na inaweza kukawa na mazingira yanayo saidia hilo.
 • - Kuna misingi ya kimalezi yenye athari za wazi.
 • - Kwa kukosekana misingi hiyo inatokea vurugu.
 • - Mwanaadamu akipata malezi mazuri atajua namna ya kupambana na changamoto.
 • - Yapasa kujenga kujiamini.
 • - Sekta ya malezi inatakiwa kuhakikisha jambo hilo linapatikana kuanzia kwa mtoto hadi mkubwa.
 • - Kujiamini hupatikana pale mtu anapokua anaweza kufanya jambo fulani.
 • - Wanaadamu wanauwezo na vipaji mbalimbali ambavyo mlezi anatakiwa kuvielekeza na kuhakikisha ananufaika navyo, miongoni mwa njia za kunufaika navyo ni kumfanya kijana huyo ajiamini na wala asijione mnyonge na dhaifu.
 • - Kama watu wakijiamini tutapata jamii inayo jiamini.
 • - Kujiamini pamoja na hima ya kufanya jambo vinatakiwa vipambwe na kuheshimu taifa.
 • - Kupenda taifa kunaweza kusababisha matatizo mengi na hilo ni jeraha sitaki kulizungumzia kwa sasa.
 • - Mtu akilelewa katika kupenda taifa tangu akiwa mdogo atakua mlinzi bora wa taifa lake.
 • - Pamoja na mazingira magumu anayo pitia ataendelea kua na matarajio, atafanya kazi katika mazingira yeyote hadi afikie matarajio yake na aonyeshe mchango wake katika jamii.
 • - Mtihani wa kweli ni pale taifa linapo pata mtihani kama tuliopata siku za nyuma.
 • - Uzowefu ulio onyeshwa na wananchi wa taifa hili ni fahari kwa kila mtu.
 • - Historia haijasahau na haitasahau kujitolea kwenu iwapo mtaiandika kwa mikono yenu.
 • - Kilicho tokea wakati ule kila mtu anajivunia.
 • - Vijana walionyesha ushujaa na ujasiri wa hali ya juu wakapigania taifa lao kwa nguvu zote na kwa kiwango cha juu kabisa kushuhudiwa katika zama hizi.
 • - Vijana hoa walilelewa katika taifa hili kwa hakika hayo ni matunda ya malezi bora hatuwezi kuyasahau.
 • - Kila mtu kwa nafasi yake, raia, serikali na taasisi hatutakiwi kusahau damu tukufu zilizo mwagika katika taifa hili.
 • - Tunatakiwa kuwaenzi mashujaa wetu kwa kuendeleza kazi waliyo fanya.
 • - Baada ya Marjaa Dini mkuu kutoa fatwa hakuna mtu anayeweza kutaja idadi halisi ya watu walio jitokeza kuitikia wito huo.
 • - Tukiwa sehemu hii tukufu mbele ya bwana wa mashahidi (a.s) tunathibitisha kutambua kujitolea kwao na tunawashukuru kulele cha kushukuru, Marjaa Dini aliwasifu kwa maneno bora zaidi.
 • - Hakika wao ndio fahari yetu, kigezo chetu, watu wetu, watoto wetu, hatuna cha kujifaharishia zaidi yao.
 • - Baada ya kujitolea kwao, hatuhitaji kutafuta mifano mingine, wao wenyewe ni mfano hai daima tutathibitisha kupitia wao na wao ni ushahidi wa wazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: