Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kimetangaza mpango wa kurusha matukio ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani kupitia vyombo vyote vya habari (luninga, redio, magazeti na mitandao ya mawasiliano ya kijamii), watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanarusha matukio ya ziara hii, na kufikisha ujumbe wake kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait kote duniani kupitia utaratibu ufuatao:
- - Kutakua na masafa ya luninga itakayo rusha matangazo bure kwa kiwango cha (CLEN) muda wote, itajikita zaidi katika kuonyesha baadhi za sehemu kama vile Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f), eneo la katikati ya haram mbili pamoja na ndani ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
- - Tutarahisisha utendaji wa wanahabari wa kitaifa na kimataifa kwa kuwapa vitambulisho maalumu vitakavyo wawezesha kuingia kila mahala kwa urahisi.
- - Watapewa habari na matukio ya haraka, yatakayo hitaji kurushwa mubashara (moja kwa moja) kwenye luninga na vyombo vingine vya habari.
- - Kuhusu mitandao ya mawasiliano ya kijamii, mtandao wa kimataifa Alkafeel umejipanga kurusha matukio ya ziara hii kupitia ripoti za habari na picha.
- - Redio ya Alkafeel ya mwanamke wa kiislamu ambayo ipo chini ya kitengo chetu imeandaa vipindi maalum kuhusu ziara hii vinavyo elezea malengo yake na namna ya kunufaika nayo.
- - Upande wa majarida, watumishi wa jarida la Swada Raudhataini pamoja na jarida la Alkafeel na Alkhamisi wamejipanga kuandika matukio mbalimbali ya ziara hii pamoja na huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru.