Usiku wa mwezi kumi na tano Shabani ni usiku bora baada ya usiku wa Lailatul Qadri… tambua ibada zake.

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi kumi na tano Shabani ni usiku bora baada ya usiku wa Lailatul Qadri, Imamu Baaqir (a.s) anasema, ikiwa imenukuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) alisema: (Aliulizwa Baaqir (a.s) kuhusu utukufu wa usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani, akasema (a.s): ni usiku bora Zaidi baada ya Lailatul Qadri, katika usiku huu Mwenyezi Mungu huwapa waja wake katika fadhila zake, na huwasamehe kwa neema zake, jitahidini kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika usiku huu, hakika ni usiku ambao Mwenyezi Mungu amejiahidi kutomnyima muombaji, maadam hajaomba maasi, nao ni usiku ambao kwetu Ahlulbait uko wazi kama alivyo jalia usiku wa Lailatul Qadri kwa Mtume wetu, jitahidini kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu na kumsifu). Usiku huu unaibada nyingi, miongoni mwa ibada hizo ni:

Kwanza: Kumzuru Hussein (a.s) nayo ni ibada bora katika usiku huu, husababisha kusamehewa dhambi, na anayetaka kusalimiana na mitume laki moja na ishirini na nne elfu basi amzuru (asome ziara hiyo) katika usiku huu, ufupi wa ziara hiyo ni: simama sehemu yenye muinuko kisha angalia kulia na kushoto halafu uangalie juu na useme maneno haya: (Asalamu Alaika yaa Abaa Abdi Llahi, Asalamu alaika wa rahmatu-llahi wa barakaatuhu), atakaye mzuru Imamu Hussein (a.s) kwa ziara hii ataandikiwa thawabu za hijja na umra, kwenye mlango wa ziara kumeandikwa kuhusu usiku huu.

Pili: Kuoga, hakika hupunguza dhambi.

Tatu: Kuuhuisha (kufanya ibada) za kuswali, kusoma dua na kufanya istighfaar, kama alivyo kua anafanya Imamu Zainul-Aabidina (a.s), imepokewa katika hadithi kua (Atakaye fanya ibada katika usiku huu roho yake haitakufa siku ambayo roho zitakufa).

Nne: Aombe dua hii iliyo pokewa na Shekh na Sayyid nayo ni sawa na ziara ya Imamu Ghaaibu (a.s) (Allahumma bihaqi lailatina wa mauludiha, wa hujjatika wa mauúdiha , alati qaranta ila fadhiliha fadhlan fatamat kalimatuka swidqan wa adlan laa mubadila likalimaatika, walaa muáqiba li-ayaatika, nuuruka muta-aliqu, wa dhiyaauka mushriqu, wal-alam nuuru fi twakhyaai daijuurul ghaaibu mastuur, jalla mauluuduhu wa karama mahtiduhu, walmalaaikatu shuhaduhu, wa Llahu naaswiruhu wa mu-ayyiduhu…) hadi mwisho wa dua.

Kuna ibada nyingi za kufanya katika usiku huu, nafasi haitoshi kueleza zote, unaweza kuangalia katika kitabu cha Mafaatihu Jinaani cha Shekh Qummiy.

Usiku huu utukufu maalumu tofauti na siku zingine, miongoni mwa utukufu wa usiku huu ni kuzaliwa kwa nuru miongoni mwa nuru za Muhammadiyya, mwezi kumi na tano Shabani mwaka wa (255h), riwaya tukufu zilikua zimesha bashiri mazazi hayo matakatifu ya mtu atakaye kuja kujaza dunia haki na uadilifu, ambaye ni Imamu Muhammad bun Hassan Almahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: