Watumishi wa kitengo cha uangalizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu ndio wanaowajibika kwa kila huduma ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya kufanikisha ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo ni miongoni mwa ziara kubwa inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu hapa Karbala.
Watumishi wa idara ya usafi, wamesafisha maeneo yote na kuondoa kila kilichastahiki kuondolewa katika siku hizi za ziara, kwa ajili ya kupanua eneo la kupita mazuwaru, na kupunguza msongamano wakati wa ziara.
Hali kadhalika sehemu zote zimetandikwa miswala (kapeti) kwa ajili ya kupanua sehemu za kupumzika mazuwaru, na watumishi wamekaa kila sehemu ya haram kwa ajili ya kuwasaidia mazuwaru na kuwaelekeza sehemu za kuingia na kutoka pamoja na baadhi ya vitengo wanavyo hitaji kuvitembelea, pia wamefungua sehemu mpya za kupita kwa ajili ya kuondoa msongamano ndani ya haram, na wamejipanga kusimamia uingiaji wa mazuwaru katika haram.
Kwa kushirikiana na kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na vitengo vingine tumeandaa sehemu nyingi za kuswali swala za jamaa ndani na nje ya haram, pamoja na kazi zote hizo kitengo kinaendelea na kazi zake za kila siku za kufanya usafi kwa kutumia mitambo na mikono, na kutandika miswala, na kuratibu swala ndani ya haram tukufu, na kuondoa uchafu unaotupwa na mazuwaru wakati wote.