Maukibu (539) zinatoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya amesema kua: Idadi ya mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shamani imefika (539) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, maukibu hizo zipo ndani ya eneo la mkoa wa Karbala zilizo adhikishwa kwa mujibu wa sharia, bado kuna makumi ya mawakibu ambazo hazija jiandikisha pamoja na nyumba zilizo fungua milango yao kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru”.

Akaongeza kua: “Maandalizi ya ziara hii yalianza mapema, tulipokea maombi kutoka kwa wawakilishi wa mawakibu, tukatoa maelekezo maalumu pamoja na kuainisha sehemu ya kila maukibu, ambapo tumezipanga katika barabara kubwa na ndogo zinazo elekea katika mji mtukufu wa Karbala, zilianza kutoa huduma zaidi ya siku mbili zilizo pita, na zitaendelea baada ya mwezi kumi na tano Shabani”.

Akasema kua: “Kwa ajili ya kua na matokeo mazuri yanayo endana na utukufu wa ziara hii, na kurahisisha utembeaji wa mawakibu na kuhakikisha hazizuwii shughuli za watu wengine, ikiwa ni pamoja na kuto watatiza mazuwaru watukufu, tulifanya vikao kadhaa kwa ajili ya kutoa maelekezo na miongozo kwa viongozi wa mawakibu”.

Akabainisha kua: “ Kawaida ya maukibu za kutoa huduma katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani hutoa chakula, vinywaji, malazi pamoja na matibabu, kila maukibu hutoa huduma wanayo taka, maukibu zimepangwa kwa kufuata utaratibu maalum uliopangwa na kitengo cha mawakibu, ikiwa ni pamoja na kuandikwa jina la kiongozi wa maukibu na kulikabidhi kwenye vyombo vya usalama vya mkoa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: