Ameokoa Iraq na mashariki ya kati: Hapa ndio paliasisi ushindi kabla ya miaka mitano.

Maoni katika picha
Siku kama ya leo (14 Shabani) wananchi wa Iraq pamoja na kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu wa zama (a.f), ni siku ya kuadhimisha mwaka wa tano tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, iliyo okoa ardhi ya Iraq na maeneo yake matakatifu kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, walio teka miji mingi katika mikoa ya kaskazini na magharibi mwa Iraq na wakatishia kuuteka mkoa wa Bagdad na mikoa ya kusini.

Fatwa hiyo tukufu ilipokelewa kwa wingi na wananchi, wazee kwa vijana walijitokeza kwenda kupigania taifa lao, ushujaa walio onyesha unafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, kila muiraq aliona umuhimu wa kuingia katika mapambano hayo, wote walikua tayali kujitolea nafsi zao kwa ajili ya taifa lao, walionyesha ushujaa na ujasiri wa hali ya juu, hakuna atakaye sahau milele, jambo hili litaendelea kufundishwa hadi vizazi vijavyo.

Watu waliotoka kuitikia fatwa hawakufanya hivyo ispokua baada ya kutambua kua dhalimu lazima ashindwe, wakapigana kwa ujasiri na wakatetemesha ardhi chini ya miguu ya adui zao, vijana wa Marjaiyya walitoa somo kali wa adui zao, Marjaa ambaye alikua na bado anaendelea kua mlezi na mlinzi wa raia wa tabaka zote katika taifa hili, naye ni hema litakalo wafunika siku ambayo haitakua na hema la kujifunika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: