Mwezi kumi na tano Shabani dunia iliangaziwa na nuru ya muokozi wake.

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi kumi na tano Shabani mwaka (255h) dunia iliangaziwa na nuru ya Mola wake kwa kuzaliwa muokozi wake Imamu Mahadi (a.f), naye anatokana na kizazi cha Imamu Hussein (a.s) katika kizazi cha Fatuma Zaharaa (a.s) na Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), imepokewa katika hadithi kua, Mtume (s.a.w.w.) alisema: (Nakubashiria ewe Fatuma Mahadi atatokana na wewe), akasema tena (s.a.w.w): (Na miongoni mwetu kuna Mahadi wa umma ambaye Issa (a.s) ataswali nyuma yake, kisha akapiga mabega ya Hussein (a.s) akasema: Mahadi wa umma atatokana na huyu). Mtume pia akasema: (Mahadi ni katika Ahlulbait…).

Kutokana na hadithi hizo ni wazi kua Imamu Mahadi ni miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), naye ni Imamu wa mwisho katika Maimamu kumi na mbili walio bashiriwa na Mtume (s.a.w.w) alipo sema: (Baada yangu watakuja makhalifa kumi na mbili wote wanatokana na makuraishi katika kizazi kitakasifu cha Fatuma Zaharaa na katika wajukuu wa Imamu Hussein Shahidi –a.s-).

Kuzaliwa kwake:

Ilikua kawaida ya bibi Hakima (mtoto wa Imamu Jawaad –a.s-) na shangazi wa Imamu Hassan Askariy (a.s), kila alipo mtembelea alikua anamuomba Mwenyezi Mungu amjalie mtoto wa kiume, bibi Hakima anasema: niliingia siku moja, nikasema kama nilivyo zowea kusema na nikaomba dua ambayo huomba, akasema: Ewe shangazi hakika yule unayeomba Mwenyezi Mungu aniruzuku atazaliwa usiku huu, ewe shangazi leo lala hapa kwani usiku wa leo atazaliwa mja bora mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ambaye Mwenyezi Mungu atahuisha ardhi baada ya kufa kupitia yeye, bibi Hakima akauliza: Nani atakaye jifungua ewe kiongozi wangu, sioni kama Narjisi anaujauzito. Imamu akasema: Narjisi na sio mwingine.

Akasema: Nikamkumbatia Narjisi na nikambusu tumboni kwake wala sikuona athari ya mimba, nikarudi kwake nikamuambia nilicho fanya na wala sijaona athari ya mimba. Akatabasamu na kusema, ikifika Alfajiri athari ya mimba itadhihiri kwako; kwa sababu mfano wake ni sawa na mama yake Mussa mimba yake haikudhihiri, na hakuna aliyejua hadi wakati wa kujifungua, kwa sababu Firauni alikua anapasua matumbo ya waja wazito kwa kumtafuta Mussa na huyu ni mfano wa Mussa (a.s) atakuja kumaliza utawala wa Mafirauni (waovu).

Bibi Hakima akasema: Niliendelea kumwangalia usiku wote akiwa amelala usingizi hadi ilipo ingia Alfajiri akashtuka na kuamka, nami nikamkumbalia, Imamu akasema: Msomee (Innaa anzalnaahu fii lailatul qadri), nikaanza kumsomea, nikamuuliza, unajisikiaje? Akasema: Limetokea jambo alilokuambia kiongozi wetu, nikaendelea kumsomea kama nilivyo ambiwa, akaniitikia mtoto akiwa bado yupo tumboni, akawa anasoma kama ninavyo soma na akanitolea salam.

Hakima akasema: Nilishangazwa na nilicho sikia, Imamu Askariy (a.s) akasema: Usishangazwe na amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika Mwenyezi Mungu huwatamkisha wototo kwa hekima, na kuwafanya kuwa hoja katika ardhi wanapokua wakubwa, kabla hajamaliza kuongea Narjisi akatoweka machoni kwangu, ikawa kama kuna pazia baina yetu, nikaenda kwa Imamu Askariy kumuuliza, akasema: rudi utamkuta palepale alipokua.

Akasema: Nikarudi baada ya muda mfupi ikatolewa pazia baina yetu nikamuona akiwa na nuru kubwa, mara nikamuona mtoto akiwa amesujudu na mikono yake kaelekeza juu huku anasema: (Ash-hadu anlaa ilaaha illa Llaha wahdahu laa shariika lahu, wa Ash-hadu anna jadiy Rasulullahi swala Llahu alaihi, wa anna abiy Amirulmu-uminina… akataja Imamu mmoja baada ya mwingine hadi akajitaja mwenyewe. Akasema: Ewe Mola nitimizie ahadi na unikamilishie jambo langu na unipe nguvu, uijaze dunia uadilifu na haki kupitia mimi…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: