Kazi zilizo fanywa na kitengo hicho katika siku za ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani na kuzaliwa kwa Imamu Mahdi (a.f) kupitia idara zake zote ni hizi zifuatazo:
- 1- Kutoa huduma ya habari kwa wanahabari wote waliopenda kurusha matukio ya ziara ya Shaabaniyya kutoka katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili.
- 2- Kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na kitengo cha kulinda nidham pamoja na walinzi wa haram mbili tukufu.
- 3- Kutoa gari za usafi kwa vituo vya usalama pamoja na gari za maji, na kugawa maji kwa mawakibu na mazuwaru.
- 4- Kutandika mazulia kwa ajili ya swala za jamaa na kupumzika mazuwaru.
- 5- Kuhakikisha taa zinawaka vizuri usiku mzima kwa kiasi ambacho zinaakisi furaha ya tukio hili.
- 6- Kuandaa mimbari kwa ajili ya vikao maalumu vya kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f).
Fahamu kua kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu pamoja na huduma hizo, kimetoa huduma ya maelekezo ya kidini kupitia vipaza sauti vilivyo enea katika uwanja huo.