Zaidi ya gari (150): Kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya kimeshiriki katika kusafirisha mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani.

Maoni katika picha
Kama kawaida ya ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni wa watu, kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya kimeandaa gari kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuweka utaratibu wa kubeba mazuwaru, kimefanya hivyo katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f).

Kimeandaa gari zaidi ya (150) zenye ukubwa tofauti, zikiwemo gari maalum zinazo beba mazuwaru kuanzia yanapo ishia mabasi hadi karibu na malalo mawili matukufu, chini ya utaratibu uliowekwa na kamati inayo simamia ziara kwa ajili ya kurahisisha uingiaji na utokaji wa mazuwaru katika mji mtukufu wa Karbala, sambamba na kuwarudisha hadi sehemu za kupandia gari baada ya kumaliza ziara, yaani huduma ya usafiri inayo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mazuwari ipo ya kwenda katika haram mbili na kurudi, na wamefanya kituo kikuu cha gari zao kwenye barabara ya (Hindiyya – Baabil), kwani barabara hiyo inamsongamano mkubwa wa mazuwaru.

Fahamu kua kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinamiliki gari za kisasa pamoja na mitambo mbalimbali inayo weza kutumika katika mazingira tofauti kwa mazuwaru wote na katika kila tukio la kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: