Kuelekeza, kuongoza na kufundisha maadili mema ni kazi muhimu inayo fanywa na kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo kimeweka ratiba maalum ya jambo hilo, ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu ni moja ya sehemu muhimu za kufanywa jambo hilo, na ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ni miongoni mwa ziara hizo, kama wanavyo hudumiwa mazuwaru wa kiume hivyo hivyo wanawahudumia mazuwaru wa kike, kitengo kimetoa mihadhara elekezi kwa mazuwaru wa kike ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mihadhara ilikua na mada mbalimbali, kulikua na mada za fiqhi, aqida na akhlaqi, pamoja na hukumu za swaumu na ibadaat, zilikua zinatolewa kwa wakati tofauti, pamoja na kuzingatia mida yenye watu wengi, kwa ajili ya kuhakikisha faida inawafikia wengi zaidi.
Mihadhara ilikua inatolewa na mashekhe wenye uwezo mkubwa wa kutoa mihadhara na kujibu maswali ya mazuwaru, kwa ajili ya kufaidika wote kulikua na nafasi ya kuuliza maswali kwa wazi na majibu kutolewa hapohapo ili wote wafaidike.