Kituo cha uzalishaji Alkafeel: Makumi ya vituo vya luninga vya ndani na nje ya Iraq vimenufaika kutokana na matangazo yetu maalum ya matukio ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani.

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kufaidika kwa makumi ya vituo vya luninga kutoka ndani na nje ya Iraq katika kutangaza matukio ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, kwa kutumia masafa maalumu ya bure yenye kiwango cha (Clean).

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Bashiri Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeweza kurusha mubashara (moja kwa moja) matukio mbalimbali katika ziara hii, picha zenye ubora wa hali ya juu, zinazo endana na mahitaji ya vituo vya luninga, matangazo hayo yalirushwa kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f) pamoja na kutoka katika masjid Sahala ambayo ni katika nyongeza mpya za matangazo mubashara ya ziara hii.

Akaongeza kua: “Hakika wataalamu wa kituo cha Alkafeel wanauwezo na uzowefu mkubwa unao wawezesha kupiga picha zinye viwango vya juu zinazo kubalika na vituo mbalimbali vya luninga, huduma hii imenufaisha makumi ya vituo vya luninga za kitaifa na kimataifa, tunatoa shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa huduma hii”.

Fahamu kua masafa iliyo tengenezwa kwa ajili ya kurusha matukio ya ziara hii ni:

E3B at 3°E
Down:11579.4 H
SR:3200
DVBS2
8PSK
FEC:3/4
HD/MPEH-4
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: