Kutokana na mafanikio ya siku za nyuma na kwa Baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) na Imamu wa zama Mahadi (a.f), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kufanikiwa kwa mpango wake wa ulinzi na utowaji wa huduma katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, imefanya kazi kwa hali na mali kufanikisha hilo.
Huduma zote zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya zimekua na mafanikio makubwa, hakuna tukio lolote la uvunjifu wa Amani lililo tokea kipindi cha ziara wala msongamano mkubwa wenye madhara, pamoja na idadi kubwa ya mazuwaru walio wasili kwa wakati mmoja.
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na wasaidizi wao wa kujitolea wamefanya kazi kwa bidii sana chini ya kauli mbiu isemayo: (Kumtumikia zaairu ni fahari yetu), kwa muda wa siku tatu mfululizo hadi kufikia kilele cha ziara kilicho kua ni usiku wa Jumapili, Atabatu Abbasiyya ilikua na ratiba maalum iliyo gawa kazi katika maeneo mengi, kuanzia ndani ya uwanja wa haram tukufu na kuandaa mazingira muafaka kwa kufanya ziara na kusoma dua, pamoja na sehemu za nje kwa namna ambayo inaendana na wingi wa mazuwaru.
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umewashukuru na kuwapongeza watendaji wote pamoja na watumishi wa Ataba zingine na mawakibu Husseiniyya na kila aliye changia mafanikio ya ziara hii.