Miongoni mwa machapisho ya kitengo cha Dini ni kitabu cha (Je unajua?).

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetao vitabu vya aina mbalimbali na ukubwa tofauti, kama vile vitabu vya Fighi, Aqida, Akhlaq na mambo ya kijamii, vikiwa vimeandikwa kwa lugha nyepesi inayo julikana kwa urahisi na kila mtu, na vimejaa ushahidi wa aya na hadithi za Mtume pamoja na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu cha (Je unajua?) ambacho kina mada za Fiqhi na Akhlaq pamoja na mambo yanayohusu jamii.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo mpya wa (Je unajua), kimekubalika sana ndani na nje ya Iraq, kimeandika mambo mengi ya kijamii yanayo gusa maisha ya nyumbani, shule na vyuoni.

Kimechapishwa mara kadhaa kutokana na kukubalika kwake, kwa sasa kinapatikana katika kituo cha mauzo cha kitengo cha dini mkabala na mlango wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, pia unaweza kukipakua kutoka katika anuani ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/index.php?iss
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: