Hafla ya wanawake ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f).

Maoni katika picha
Katikati ya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waliojaa furaha, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya ya Atabatu Abbasiyya imeratibu hafla wa wanawake ndani ya moja ya sardabu za Ataba, kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Hujjat bun Hassan (a.s).

Hafla hii ni miongoni mwa utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kusherehekea tukio hili, baada ya kufunguliwa kwa Quráni tukufu ikafuata khutuba ya ukaribisho iliyo tolewa na wasimamizi wa hafla hiyo, halafu zikatolewa mada mbalimbali kuhusu Imani ya kuwepo kwa Mahadi pamoja na kuelezea mambo muhimu yaliyo tokea wakati wa kuzaliwa kwa Imamu wa zama (a.f), sambamba na kutaja baadhi ya hadithi tukufu zinazo mzungumzia.

Hafla ilipambwa na kaswida pamoja na mashairi mbalimbali yaliyo taja utukufu wake, mwisho kila mtu aliinua mikono juu na kuomba Mwenyezi Mungu amlete haraka Imamu wa zama, na alinde taifa letu pamoja na maeneo matakatifu bila kuwasahau Maraajii wetu watukufu, na awarehemu mashahidi wetu na kuwafufua pamoja na Mtume Muhammad na Aali Muhammad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: