Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu unashiriki katika hafla ya ufungaji wa kongamano la (Baqiyatu Llah) katika Masjid Sahala tukufu.

Maoni katika picha
Kwa kuhudhuria kundi kubwa la wasomi wa Dini na sekula pamoja na wawakilishi wa Ataba na mazaru takatifu, ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika hafla ya kufunga kongamano la (Baqiyatu Llah) la kumi na mbili, lililo simamiwa na uongozi wa Masjidi Sahala kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baqiyatu Llah Imamu Hujjat Almuntadhir (a.f) iliyo fanyika mwezi kumi na tano Shabani (1440h).

Katibu mkuu wa Masjid Sahala Mhandisi Mudhar Sayyid Ali Khaan Almadaniy katika khutuba yake amesema kua: “Hakika kukutana kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wa ajili ya kuadhimisha tukio hili, ni kukutana kwa nyoyo zinazo ungana katika kuonba aje haraka Imamu wa zama (a.s), kongamano la Baqiyatu Llah ni jambo dogo sana tunalofanya kuhusu tukio hili”.

Akasisitiza kua: “Hakika utukufu wa leo siku aliyo zaliwa mkombozi wa wanaadamu wote, watu wote kuanzia Adam (a.s) hadi Mtume Muhammad (s.a.w.w), pamoja na mawalii watakasifu wanaisubiri siku iliyo ahidiwa ya muokozi mtukufu, atakayejaza dunia amani na uadilifu baada ya kujaa dhulma na uovu, akazungumza baadhi ya riwaya kuhusu ubora wa Masjid Sahala, na akawashukuru watu wote waliohudhuria kutoka katika Ataba mbalimbali na mazaru za kishia, akamtaja Alamah marehem Sayyid Muhammad Ali Halo, aliyekua amezowea kuhudhuria kongamano hili na kuwasilisha mada za kitafiti kuhusu Imamu wa zama (a.f).

Hafla ilipambwa na mashairi, tenzi na maigizo. Pembezoni mwa hafla hiyo kulikua na maonyesho ya kazi za mikono.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu imezowea kuhudhuria mahafali na makongamano mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano pamoja na Ataba na mazaru za kishia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: