Rais wa kamati tendaji ya kufuta ujinga katika wizara ya malezi amesema kua: Hakika kujali kwa Atabatu Abbasiyya tukufu swala la kufuta ujinga ni dalili kua inajali jamii.

Maoni katika picha
Rais wa kamati ya kufuta ujinga katika wizara ya malezi Dokta Hafadhi Rashidi Halbusi amesema kua; kuguswa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na swala la kufuta ujinga ni dalili kua inajali jamii.

Ameyasema hayo katika khutuma aliyo toa kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la kufuta ujinga, linalo simamiwa na kamati tendaji ya kufuta ujinga katika wizara ya malezi kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapigajani pamoja na ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, lilifanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya na litadumu siku tatu.

Akaongeza kua: “Ni furaha na fahari kubwa leo kua pamoja nanyi, tunafanya kazi pamoja ya kupambana na ujinga, natoa shukrani za dhati kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala na kila aliye shiriki kufanikisha kongamano hili, hii ni dalili ya wazi kua Atabatu Abbasiyya inatambua hatari ya ujinga (kutojua kusoma na kuandika) katika jamii.

Akaendelea kusema kua: “Hakika umuhimu wa kufuta ujinga sio wa serikali peke yake, hili ni swala la kibinaadamu, kijamii na kisheria, linahitaji nguvu za pamoja, tunatakiwa kushirikiana wote, taasisi za serikali, raia, dini, wahadhiri wa vyuo vikuu, wahadhiri wa Husseiniyyaat, wazee wa makabila, kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa apambane kuondoa ujinga, na hivyo ndio sheria ya kuondoa ujinga inavyosema”.

Halbusi akafafanua kua: “Sheria ya kufuta ujinga namba 23 ya mwaka 2011m imezungumza swala la kushirikiana katika kupambana na janga la ujinga (kutojua kusoma na kuandika) katika jamii, ni wazi kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ujinga, ugaidi na ufakiri, hivyo ni jukumu letu sote kupambana na janga hilo, na kuiokoa jamii isidumbukie katika maafa ya ujinga, tunasisitiza pia umuhimu wa kuendelea kushirikiana na taasisi za kimataifa zenye uzowefu na swala hili kama vile Unesco”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunarudia kushukuru kwa dhati Atabatu Abbasiyya kwa kuwa mwenyeji wa kongamano hili ambalo tunategemea kufikia malengo yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: