Kwa mara ya kwanza kuingizwa katika orodha ya vyuo: Chuo kikuu cha Alkafeel kimepata nafasi ya (19) katika orodha ya vyuo vya serikali na vya binafsi.

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeingizwa katika orodha ya vyuo vikuu vya kimataifa kwa mara ya kwanza, na kupata nafasi ya kumi na tisa (RUR - Round University Ranking) katika ubora wa kitaifa ulio shindanisha vyuo vikuu vya serikali na binafsi hapa Iraq, na ikapana nafasi ya (819) katika vyuo vikuu vya kimataifa.

Uongozi wa chuo umesema kuingia katika orodha hiyo ni hatua ya kwanza katika mkakati wa chuo chini ya wizara ya elimu ya juu, na kuhakikisha tunatoa elimu bora.

Kumbuka kua utaratibu wa kushindanisha ubora wa vyuo (RUR - Round University Ranking) ni utaratibu wa kimataifa, unajumla ya vyuo (930) katika nchi (80), wanaangalia vipengele 20 katika mambo 4 makuu ambayo ni: Ufundishaji, Utafiti, Mchanganyiko wa mataifa, kuwa na vitega uchumi endelevu. Hulenga kupata taarifa kamili kuhusu uwezo wa chuo katika kutatua changamoto za wanafunzi, jamii ya wasomi, uongozi wa chuo, na muundo wa siasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: