Vikao vya kujadili mikakati ya kupambana na ujinga bado vinaendelea

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Kupambana na Ujinga ni jukumu la wote) siku ya pili mfululizo, vikao vya kujadili mbinu za kufuta ujinga vinavyo simamiwa na kamati tendaji ya kufuta ujinga katika wizara ya malezi ya Iraq kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s) pamoja na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya bado vinaendelea, vimefanyika vikao kadhaa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) vya kujadili mikakati ya kufuta ujinga.

Mijadala imeongozwa na jopo la wasomi walio bobea katika mambo haya, ambapo wamejadili njia zinazo tumika kufundisha watu wakubwa, na mikakati inayo andaliwa kutekeleza jambo hilo, yametolewa maoni mbalimbali ya namna nzuri ya kupambana na tatizo la ujinga linalo ikumba jamii ya wairaq, ukatolwa wito wa kua na mkakati shilikishi utakao husisha wananchi wote wa rika tofauti.

Pia tumeangalia uzowefu wa taasisi zinazo fanya kazi ya kupambana na ujinga, kwa mfano Atabatu Abbasiyya tukufu na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, ambao wanamafanikio makubwa katika kazi hiyo pamoja na changamoto wanazo pata, na kuiomba serikali ya Iraq iweke mkakati wa kitaifa utakao saidia kufuta ujinga unao enea kwa wananchi wa Iraq watoto na vijana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: