Kufanyika makongamano ya kuhuisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f) kunaonyesha namna jamii inavyo fungamana naye.

Maoni katika picha
Ustadh Mahadi Ashiki kutoka uturuki amesisitiza kua kufanya mikutano ya kuhuisha kuzaliwa kwa Imamu Muhadi (a.f) kunaonyesha namna jamii ilivyo fungamana naye (a.s).

Ameyasema hayo katika khutuba aliyo toa kwenye hafla ya ufunguzi wa awamu ya kumi ya kongamano la utamaduni wa amani, lililo fanyika Alasiri ya Jumatano (18 Shabani 1440h) sawa na (24 April 2019m) katika mji wa Diwaniyya, chini ya usimamizi wa taasisi ya Imamu Swadiq (a.s) kwa kushirikiana na Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya).

Akaongeza kua: “Lakufurahisha zaidi waliohudhuria katika tukio hili tukufu, ni wanachuoni na viongozi wakubwa wa mji huu wa Imamu Mahadi (a.f)”.

Akasisitiza kua: “Hakika kufanyika kwa mikutano kama hii kwa namna hii, kunaonyesha kua wanachuoni wa mji huu wanashauku kubwa ya kuitumikia Dini tukufu, na kunaonyesha juhudi kubwa zinazo fanywa na Ataba tukufu hapa Iraq, kwa kusaidia jambo lolote la kumtumikia mwanaadamu pamoja na kuonyesha mafungamano makubwa yaliyopo kati ya jamii na Imamu Mahadi (a.f), mafungamano yanayo taka kuondolewa na maadui”.

Akabainisha kua: “Kukutana watu wa aina tofauti katika kongamano hili kunaonyesha wazi utekelezaji wa amri ya Aali Muhammad (s.a.w.w), ambao ukamilifu, baraka na mafanikio ya umma huu yanatokana na wao”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mkusanyiko huu auonyeshe dola tukufu, itakayo ongozwa na taifa hili chini ya bendera ya Baqiyatu Llah (a.f) hakika wao wanaiona ni mbali na sisi tunaiona ni karibu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: