Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesisitiza ulazima wa kusaidia raia wa Iraq katika sekta zote ikiwa ni pamoja na sekta wa mawasiliano.

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amesisitiza umuhimu wa kuwasaidia raia wa Iraq katika sekta zote muhimu kwa ustawi wa uchumi.

Ameyasema hayo alipo tembelea makao makuu ya shirika la mawasiliano Alkafeel, akiwa na jopo la watumishi wa Atabatu Abbasiyya wakiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi (d.t), wakapokelewa na kiongozi mtendaji Mhandisi Aarifu Bahashi.

Kiongozi mkuu wa kisheria ameonyesha imani kubwa kwa shirika hilo ambao linatumia watalamu wa nchini na mtaji wa ndani kwa asilimia (%100), wanafanya kazi kwa kufuata utaratibu uliopangwa na watalamu walio bobea katika sekta hii, pamoja na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa uhandisi wa mawasiliano, kwa ajili ya kuandaa rasilimali watu ya kutosha yenye uwezo wa kuendeleza kazi hizi kwa ufanisi mkubwa kila sehemu ya taifa letu kipenzi, kwa namna ambayo itawezesha kupata huduma ya mawasiliano kwa wananchi wote wa Iraq kwa kiwango cha kitaifa na kimataifa.

Mheshimiwa amehimiza kujikita katika kusaidia vijana na kuendeleza vipaji vyao katika mambo mbalimbali ya kielimu, kwa ajili ya manufaa ya shirika na taifa kwa ujumla, kufanya hivyo kutadumisha mafanikio na kuendelea kutegemea akili za raia wa Iraq watu ambao hakuna asiyejua uwezo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: