Idara ya wanawake yazindua maonyesho katika chuo kikuu cha Karbala.

Maoni katika picha
Idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia harakati zake za kiutamaduni, imezindua maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Karbala/ kitivo cha elimu za kiislamu, maonyesha haya yanafanywa kwa mara ya kwanza na yanatarajiwa kufanywa katika vyuo vikuu vingine pia.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya wanawake bibi Asmaa Raádu kwa mtandao wa Alkafeel, Yanafanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Kitabu ni utamaduni wa kudumu na kusoma ni turathi ya asili) kuna karibu aina (300) za vitabu kutoka kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha malezi na elimu ya juu, yanaingia katika harakati za kitamaduni ya aina yake, sambamba na kuwepo kwa aina tofauti ya vitabu vinavyo shiriki maonyesho haya, kuna vitabu vya watoto, wanafamilia na wanautamaduni miongoni mwa wanafunzi na walimu. Maonyesho haya yanakusudia kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi ya kujua umuhimu wa elimu na kusoma.

Bibi Lamyaau Mussawi mmoja wa wasimamizi wa fikra ya maonyesho ya vitabu akasema kua: “Hakika maonyesho yamekamilika yana vitabu vya aina tofauti, yanawakilisha harakati inayo ongea ya akili na kutoa fursa ya kupima fikra za waandishi na utamaduni alisi, pia ni fursa ya kuimarisha mawasiliano kwa wasomi na taasisi za malezi na elimu pamoja na za kijamii na nyinginezo”.

Wakufunzi wa masomo ya kiislamu katika chuo wamesema kua: “Hakika maonyesho ya vitabu ni hatua nzuri na muhimu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuelekeza akili za wanafunzi katika vitabu ambavyo ni chakula cha fikra na roho, pia ni jambo zuri ya kulea uwezo wa mwanafunzi sambamba na kuwafanya wapunguze matumizi ya mitandao ya kijamii”.

Pembezoni mwa maonyesho hayo kimefanyika kikao cha kutambulisha ofisi nne katika idara ya wanawake, ambazo ni: (ofisi ya elektronik, ofisi ya usomaji, ofisi ya kurudufu na ofisi ya faharasi), kila ofisi ilieleza kwa ufupi majukumu yake.

Kumbuka kua maonyesho haya yanafanyika kwa sababu kusoma ndio njia pekee ya kulea akili na kuongeza maarifa, baada ya kuwepo kwa mitandao mingi ya mawasiliano ya kijamii usomaji wa vitabu umeshuka hasa kwa vijana, kwa hiyo Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia maonyesho haya kama njia ya kuhamasisha usomaji wa vitabu kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: