Kituo cha utamaduni wa familia ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kuanzishwa kwake kimejikita katika kuangalia matatizo ya familia na kusaidia utatuzi wake, kinatumia njia mbalimbali katika kutatua matatizo hayo, na kinatoa mafunzo kwa wanajamii kuhusu jinsi ya kujiepusha na matatizo ya kifamilia, kinalenga watu wa tabaka tofauti na kinaprogram maalum ya tabaka la wanafunzi wa vyuo, kwani wao ni moja ya nguzo muhimu katika jamii, katika kutekeleza hilo hutumia program tofauti ikiwemo program ya (funguo za Saáda).
Program hii huendeshwa kwa kushirikiana na wakuu wa vyuo kwa ajili ya kuhakikisha haitatizi ratiba za masomo kwa wanafunzi, na imeanzia katika chuo kikuu cha Karbala, imefanya kikao cha kwanza katika chuo hicho, kilicho kua na mawaidha elekezi pamoja na kutoa nafasi ya maswali na majibu, mwisho wanafunzi waliulizwa maswali na zawadi zikatolewa kwa waliojibu vizuri.
Kikao kimepata mwitikio mkubwa wa wanafunzi na wameonyesha kufurahishwa na program hii, wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia kilichopo katika jengo la Swidiiqah Twahirah mtaa wa Mulhaq katika mji mtukufu wa Karbala, kimebobea katika mambo ya familia, kilianzishwa kwa ajili ya kusaidia kutatua matatizo ya kifamilia hapa Iraq, na kusaidia kuweka amani na utulivu wa nafsi katika familia, hutoa mafunzo ya nafsi kwa wanafamilia wa rika zote na hufuatilia mafundisho yake kupitia kamati maalum ya watalamu na kwa utaratibu maalum.